1. Chunga wako mdomo,
Uombao kila kitu,
Walowahi omba na kuonja,
Hawasiti kusifia,
Yao kiu wamekata,
Kwa maji ya ajabu,
Maji hayo asilia,
Chemichemi adimu,
Yapo tokea enzi,
Wenye ndevu huyateka.
2. Vitu vingi tumeonja,
Hata visivyohesabika,
Vyenye utamu wa asali,
Na uchungu wa shubiri,
Pia vyenye ukakasi,
Na vilosheheni uchachu,
Hebu swali jiulize,
Radha ipi ni bora?
3. Katikati ya nyika,
Yenye miti miwili,
Kuna kisima cha ajabu,
Chapakana na milima,
Kingo zake raini,
Kila wakati zagongana,
Juu yake kuna nyasi,
Maji yake mruwa,
Wenye kata huyateka.
4. Nusu mita toka kisimani,
Pana matunda mawili,
Yalosimama wima,
Mithili ya vichuguu,
Yote yatoa unyevu,
Majira ya masika,
Pembezoni mwa kisima,
Pana sehemu tambarare,
Maji yanapopampiwa,
Cha ajabu pafurika!
5. Nyasi ndefu zafyekwa,
Kisima wazi mwituni,
Kikingojea watekaji,
Kiu yao kuikata,
Utamu usoelezeka,
Heko jalali kukiumba,
Kisima kisichonyauka,
Toka zama za mababu.
6. Wamiliki wa kisima,
Hakika wana masharti,
Kuonja yake maji,
Mpaka uwe na pampu,
Tena iliyo imara,
Kisimani utumbukize,
Pumzi ukishindilia,
Uvute maji matamu,
Lo! Kisima hiki cha enzi,
Koho laburudika!
0 comments:
Post a Comment