For Proofreading, Copy-editing, Substantive Editing of Research or Conference Papers, Reports, Manuscripts, Thesis; call: +255 716 23 1772 or E-mail: jaba@udsm.ac.tz

Dira (Sehemu ya Kwanza)


Tumo ndani ya bahari, tunaongozwa na dira,
Abiria jihadhari, akijalizwa king’ora,
Majini kuna hatari, waweza pata hasara,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

Hebu ndege tazameni, Dira ndiye  Kiongozi,
Ingawa kuna rubani, bila dira haiwezi,
Kweli tumo safarini, hili naliweka wazi
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

Elimu ni kama dira, itutowayo gizani,
Ili tuzidi kung’ara, popote ulimwenguni,
Ujinga una madhara, waleta umaskini,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

Wanafunzi na Walimu, na wanavyuo wenzetu,
Zingatieni elimu, Dira ya vizazi vyetu,
Wanazuoni kwa zamu, tufunze jamii zetu,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment