For Proofreading, Copy-editing, Substantive Editing of Research or Conference Papers, Reports, Manuscripts, Thesis; call: +255 716 23 1772 or E-mail: jaba@udsm.ac.tz

Dira (Sehemu ya Pili)


Najua unaelewa, mola hutoa umbile,
Wapo walopungukiwa, na hawakupenda vile,
Msiwaache wakiwa, na kuwatenga milele,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

Walemavu kuwajali, ndiyo iwe yetu jadi,
Misaada mbalimbali, wapeni wao zaidi,
Kwao tusiwe wakali, katu tusiwakaidi,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

Ona watoto yatima, wanaranda mitaani,
Hawana baba na mama, waona giza mbeleni,
Siwapite wima wima, nilichonacho wapeni,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo

Maisha yana utata, maringo yako ya nini?
Mbele sawa na karata, wathamini maskini,
Si vizuri kuwaita, watoto wa mitaani,

Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.
Wapo wagangao njaa, bila ya utaratibu,
Wazunguka kama saa, bila hata wajibu,
Si kila kinachong’aa, ukadhania dhahabu!,
Hii ndiyo dira yetu, kubali wake mwongozo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment