Pindi wana-kukirimu, lengo lao walijua?
Utajihisi muhimu, mabaya hutodhania,
Maneno yao matamu, fisadi hutong’amua,
Kwa fadhira za msimu, baadae wajutia,
Takrima ni adui, sawa na kidudu mtu.
Chujio likiwadia, koboko naye ni mwema,
Watu atuzawadia, bila kuleta kiama?!,
Siku akijishindia, katu hatoi huduma,
Anyata kwa kudundia, huku sumu akitema,
Takrima ni adui, sawa na kidudu mtu.
Usiku wabisha hodi, takrima mkononi,
Wajifanya ni zawadi, eti wanakuthamini!,
Kwa mtizamo jadidi, wana siri kibindoni,
Wakugeuze mradi, siku hizo za usoni,
Takrima ni adui, sawa na kidudu mtu.
Hakika hii si ofa, bali ni hofu yaleta,
Wa hivi wanakifafa, wana-kaya mtasota,
Baadaye ni maafa, wenyewe mtayapata,
Mwapaswa kuziba nyufa, msijejenga ukuta,
Takrima ni adui, sawa na kidudu mtu.
Yatupasa kuwabeza, mbeleni watatukwaza,
Takrima yatutweza, wazalendo twapooza,
Hebu jaribu kuwaza, kabla ya kujiponza,
Kwani chema chajiuza, kibaya chajitembeza!
Walimwengu tuwe macho, kuepusha dukuduku
0 comments:
Post a Comment