Naililia dunia, wapi inaelekea?
Mwovu hutomnunia, kwani atakuchekea!
Mwizi hutomdhania, jinsi anavyoongea!
Shetani amepania, utambi kutuchomea,
Kweli hiki ni Kiama, je Wangapi watapona?
Nazo nyumba za wageni, sasa hazitamaniki,
Makahaba kwa wahuni, waingizana lukuki,
Yatendekayo gizani, mengi hayasimuliki,
Wakaao vijiweni, kwa bangi hawambiliki,
Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?
Mabinti watoa mimba, bado ngono hawaachi,
Watoto wadhani pumba, watupa bado wabichi,
Mola alichokiumba, waondosha kwenye nchi,
Wazidisha kujipamba, kwa kuvaa nusu uchi,
Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?
Penzi la jinsia moja, mjini limeshamili,
Jamii yajikongoja, usodoma wavinjali,
Usaganaji si-tija, wapotosha maadili,
Ushoga pia nataja, wamchukiza jalali,
Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?
Wanandoa wenye hati, hawadumu kwenye ndoa,
Uzinzi na kurawiti, nasaha zatiwa doa,
Ufumanizi gesti, huko bandika bandua,
Kuvuta mihadarati, dhambini twajongea,
Kweli hiki ni kiama, wangapi watapona?
Wanaume wafunga ndoa, wanawake vilevile,
Kanisa la shadidia, wawe pamoja milele!
Kwa mola hili ni doa, toka zamani za kale,
Muhimu kuliondoa, lisifikie kilele,
Kweli hiki ni kiama, wangapi watapona?
Useja pia usimbe, jamii yakumbatia,
Kwenye ulevi wa pombe, vijana watumbukia,
Ushabiki wa kipambe, wagubika familia,
Pasipo mbinu kabambe, taifa laangamia,

0 comments:
Post a Comment