For Proofreading, Copy-editing, Substantive Editing of Research or Conference Papers, Reports, Manuscripts, Thesis; call: +255 716 23 1772 or E-mail: jaba@udsm.ac.tz

Kiama (Sehemu ya Pili)

Chunguza kwenye Umati, Uvaaji unatisha,
Picha za uasherati, sinema zinaonesha,
Soma kwenye magazeti, ulimwengu umekwisha,
Chungulia intaneti, vijana zawapotosha,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?

Chanzo cha ‘homosekisho’, mie chanitatanisha,
Weupe ndio fundisho, kwa nini watudunisha,
Wafrika iwe mwisho, mila zetu zatutosha,
Na tuweke ukumbusho, wanetu kuwafundisha,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?

Magonjwa sasa asidi, wanadamu hatuoni,
Majanga nayo yazidi, vizazi vi-matatani,
Mazingira twakaidi, jua liko utosini,
Tudumishe tufaidi, la sivyo tumo jangwani,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?

Ukahaba wanawili, danguro zaongezeka,
Labda wana vibali, nani wakunung’unika?
Ingawaje hatujali, wanafunzi wahusika,
Japo twaficha ukweli, wote tunaadhirika,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?

Pande nne duniani, tumshujudu manani,
Baibo na Kuruani, zitupe matumaini,
Zinayo hekima ndani, pamoja tujifunzeni
Tusije pata huzuni, duniani na mbinguni,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?


Sheria zifanye kazi, kwa watiwao nguvuni,
Nawe uliye mzazi, piga upatu bungeni,
Shiriki ngazi kwa ngazi, wafike mahakamani,
Watwaribia vizazi, kwa miigo uzunguni,
  Kweli hiki ni kiama, je wangapi watapona?

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

0 comments:

Post a Comment